Dirisha
la uchaguzi la majira ya joto barani Ulaya linaendelea kupamba moto na
tayari kuna usajili wa mamilioni ya pauni unaohusisha wachezaji wenye
majina makubwa umefanyika. Tayari miamba ya soka Uhispania klabu ya
Barcelona imemsajili msahmbuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann kutoka
klabu pinzani ya Atletico Madrid kwa kitita cha euro milioni 120.
Atletico kwa upande wao wametumia kitita cha pauni milioni 126 kumsajili Joao Felix mwenye miaka 19 kutoka Benfica ya Ureno.
Lakini
kama ilivyokuwa katika misimu iliyopita, kuna nyota wakubwa ambao
wanataka kuhama ama wanahusishwa na uhamisho wa pesa nyingi lakini mpaka
sasa bado hakuna kilichofikiwa.
Kuna nyota watatu, ambao
wanaonekana kusaka uhamisho kwa nguvu zote. Nyota hao wamegoma kuungana
ama wameachwa na tmu zao katika kipindi hichi cha kujiandaa na msimu
mpya wa 2019/2020.
Laurent Koscielny
Huyu ni nahodha wa washika bunduki wa London klabu ya Arsenal.
Koscienly
mwenye miaka 33 alijiunga na Arsenal mwaka 2010 na bado yungali na
mkataba na klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu wa 2019/2020.
Hata hivyo ameweka wazi nia yake ya kutaka kuondoka klabuni hapo katika dirisha hili la usajili.
Nahodha
huyo ameenda mbali kwa kufikia hatua ya kugoma kusafiri na timu kwenye
kwenye ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.
Katika
taarifa kwa vyombo vya habari, Arsenal imeeleza kusikitishwa kwake na
hatua hiyo ikisema ni “kinyume kabisa na maelekezo yetu kwa mchezaji.”
Klabu tatu za nchini Ufaransa Bordeaux, Rennes na Lyon zimeonesha nia ya kutaka kumsajili mchezji huyo.
Inaarifiwa kuwa Bordeaux imempa ofa ya mkataba wa miaka mitatu.
Mchezaji
nyota wa zamani wa Arsenal, Ian Wright amemtahadharisha Koscienly kuwa
matendo yake ya sasa yatamfanya afute kumbukumbu zote nzuri
alizojijengea kwenye mioyo ya mashabiki wa Arsenal kwa miaka 9.
Matthijs de Ligt
Image captionMatthijs de LigtDe Ligt naye ni nahodha na hajaungana na timu yake kwenye kambi ya maandalizi na anasaka uhamisho kwa nguvu kama Koscienly.
Tofauti baina yao ni kuwa, De Ligt ana baraka zote kutoka uongozi wa Ajax juu ya kile afanyacho.
Ajax
kwa sasa wapo kwenye kambi ya maandalizi nchini Austria na nahodha wao
amebaki Amsterdam akisubiri kukamilika kwa uhamisho kwenda moja ya klabu
kubwa Ulaya.
Beki huyo wa kati kisiki ni kinda kiumri, ana miaka
19 tu, lakini ameiongoza Ajax kuchukua ubingwa wa Uholanzi msimu
uliopita na kufika fainali ya klabu bingwa Ulaya ambapo walifubgwa na
Liverpool.
De Ligt anawindwa na Barcelona, Juventus, Manchester United na Paris St-Germain.
Wiki iliyopita, rais wa klabu ya Barcelona Josep Bartomeu alisema anajua wapi mchezaji huyo atacheza msimu ujao.
Machampioni
wa Italia klabu ya Juventus wanatajwa kuwa ndio wanaoweza kuinasa saini
ya beki huyo na wanatarajiwa kutoa kitita cha pauni milioni 71.
Mauro Icardi
Tofauti na De Ligt na Koscienly, Icardi alivuliwa unahodha wa klabu yake mwezi Februari mwaka huu.
Icardi
naye hayupo kwenye kambi ya maandalizi ya Inter Milan na mshambuliaji
huyo anatarajiwa kuuzwa kwenda klabu nyengine hivi karibuni.
Kama ilivyo kwa De Ligt Icardi amekubaliana na uongozi wa klabu hiyo kutokuwa sehemu ya kambi ya maandalizi.
Juventus ndiyo imekuwa ikitajwa zaidi katika mbio za kumsajili lakini mpaka saasa hakuna mazungumzo rasmi yaliyofanyika.
Napoli
pia wanahusishwa na kumtaka sawia na AS Roma japo itakuwa vigumu kwa
Icardi kwenda Roma ambao hawatashiriki Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.
Pogba na Lukaku
Alipoulizwa
na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita juu ya mustakabali
wake katika kikosi cha Man United, Lukaku akajibu: “subirini wiki ijayo
mtajua kitu.”
Lukaku amekuwa akihusishwa na kuhamia katika klabu
ya Inter Milan, na imefahamika kuwa uhamisho wake utategemea na
kitakachotokea kwa Icardi. Lukaku anapaswa kuondoka Man United
Hivyo endapo Icardi atauzwa wiki hii, ni dhahiri kuwa uhamisho wa Lukaku kujiunga na klabu hiyo utakuwa umeiva.
Lukaku
ameambatana na kikosi cha United kwa sasa kilichopo kwenye ziara ya
maandalizi ya msimu mpya nchii Australia na Singapore.
Mshambuliaji huyo hakuwa na wakati mzuri msimu uliopita na amekuwa akishutumiwa kwa kushuka kiwango. Kwa
upande wa Pogba kumekuwa na sarakasi za kutosha na zilikolea pala
mchezaji huyo aliposema mwezi uliopita kuwa ”sasa inaweza kuwa muda
mzuri wa kuhamia sehemu nyingine”.
Ni dhahiri kuwa si kocha Ole
Gunnar Solskjaer wala uongozi wa Man United unaotaka mchezaji huyo nyota
kuondoka Old Trafford katika dirisha hili la usajili la majira ya joto.
Wiki
iliyopita, wakala wa mchezaji huyo Raiola aliliambia gazeti la The
times kuwa mchezaji wake anataka kuondoka, na klabu hiyo inajua fika nia
ya mteja wake.
Vilabu vya Real Madrid na Juventus vinaripotiwa
kutaka kumsajili kiungo huyo Mfaransa mwenye miaka 26 japo hakuna kati
yao ambaye amepeleka maombi rasmi ya kutaka kumnunua.
0 comments:
Post a Comment