REAL
Madrid ipo kwenye mpango wa kuwauza nyota wake watano ili kupata pauni
milioni 200 kwa ajili ya kumnunua kiungo wa Manchesster United, Paul
Pogba.
Nyota huyo raia wa Ufaransa anahusishwa kujiunga na Real Madrid ambao wapo kwenye hekaheka za kuipata saini yake.
Inaelezwa
kuwa Madrid inatazamia kuwauza Gareth Bale, James Rodriguez, Dani
Ceballos, Marco Asensio na Isco ili kukusanya mkwanja huo.
Atletico Madrid na Napoli zinahitaji kumpata Rodriguez huku Arsenal na Tottenham zikiwania saini ya Ceballos.
Asensio
na Isco bado wanatazamwa kama wanaweza kuingia kwenye mipango ya Real
Madrid ila haijawa wazi kama meneja, Zinedine Zidane ana mpango nao
msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment