Monday, September 23, 2019

Bernardo Silva and Benjamin Mendy
Ujumbe wa twitter uliotumwa na Bernardo Silva kwa mchezaji mwenza wa timu ya Manchester City, Benjamin Mendy unachunguzwa na shirikisho la soka kwa kutuhumiwa kuwa wa ubaguzi.
Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno Silva alimlinganisha Mendy na kibonzo cha rangi ya chakuleti kwenye pakiti ya pipi ya Conguitos - zinazopatikana Uhispani na Ureno.
Ujumbe huo uliwekwa Jumapili mwendo wa saa tisa kasoro robo mchana na ukafutwa mwendo wa saa tisa na nusu.
Baadaya hapo Bernardo alituma ujumbe mwingine kwenye twitter: "Huwezi hata kufanya mzaha siku hizi na rafiki yako."
Mashabiki walijibu kwa kutaka ujumbe huo ufutwe.
Mmoja aliandika "Mshkaji, amekutusi kwa ubaguzi wa rangi." Mwingine aliandika: "Bernado Silva ameandika ujumbe gani?"
Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Mendy na Silva ni marafiki wa karibu na wameichezea MOnaco pamoja kabla ya wote kujiunga na City mnamo 2017.
Mendy alijibu ujumbe huo na hakuonekana kuhisi vibaya.
Manchester City imekataa kutoa tamko kuhusu hilo.
FA litaukagua ujumbe huo na msingi wa kwanini uliandikwa hadharani kabl aya kuamua hatua ya kuchukua.

0 comments:

Post a Comment