Friday, November 1, 2019




MIRAJ Athuman, nyota wa Simba amesema kuwa anajivunia kuwa karibu na John Bocco pamoja na Meddie Kagere kwa kuwa wanampa ujuzi unaomfanya azidi kujiamini.

Miraj ametupia jumla ya mabao manne ndani ya Simba akiwa nyuma ya kinara wa utupiaji Meddie Kagere mwenye mabao saba.

Miraj amesema: "Uwepo wa Kagere na Bocco ndani ya Simba unazidi kunijenga na kunikomaza kwani hawa wote wawili wana ujuzi kuliko mimi najivunia uwepo wao.

"Mara kwa mara wamekuwa wakiniambia maneno ambayo yananijenga na kunipa hasira ya kupambana kutafuta matokeo," amesema.

0 comments:

Post a Comment