Real
Madrid wanaangalia uwezekano wa kutoa malipo makubwa kuwahi kushuhudiwa
ya pauni milioni 340 kwa ajili ya mchezahi wa safu ya mashambulio wa
Paris St Germain mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappe. (Le Parisien via
Calciomercato)

Huo utakuwa usajili mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya soka kwa kuwa anayeshikilia rekodi ni Neymar ambaye alisajiliwa kwa dau wa pauni milioni 200 wakati Ronaldo akienda Juventus kwa pauni milioni 105.
Cristiano Ronaldo hatalipishwa faini na Juventus kutokana na mienendo aliyoonyesha baada ya kutolewa uwanjani na badala yake kuwekwa mchezaji wa ziada katika mchezo wa pili.
Ingawa mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 34, atatarajiwa kuomba msamaha kwa wachezaji wenzake. (Gazzetta dello Sport, in Italian)

Rais wa klabu ya Napoli Aurelio de Laurentiis amepokea Euro milioni 560 kwa ajili ya Ligi ya klabu ya Serie A kutoka Qatar huku mashabiki wakipinga na wachezaji wakigoma . (Mail)

Nemanja Matic anataka kuondoka Manchester United ikiwezekana mwezi Januari
Tottenham wanatarajia kumchukua mshambuliaji wa kati wa timu ya Roma ya Italia Lorenzo Pellegrini, mwenye umri wa miaka 23, kama mtu anayeweza kuchukua nafasi ya Christian Eriksen. (Football Italia)
Nemanja Matic anataka kuondoka Manchester United, ikiwezekana mwezi Januari, huku kiungo huyo wa kati Mserbia mwenye umri wa miaka 31 akitarajiwa kwenda Italia. (telegraph)
0 comments:
Post a Comment