
Real Madrid
wanaangalia uwezekano wa kutoa malipo makubwa kuwahi kushuhudiwa ya
pauni milioni £340 kwa ajili ya mchezahi wa safu ya mashambulio wa
Paris St Germain mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappe. (Le Parisien
via Calciomercato)
Unaweza pia kusoma;
- Raia wa Tanzania kuanza kujipima wenyewe virusi vya ukimwi
- Raia wa Marekani anayeshukiwa kuwa mfuasi wa IS akwama 'mpaka wa Uturuki'
- Zijue athari za sumu kuvu mwilini
Ingawa mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 34, atatarajiwa kuomba msamaha kwa wachezaji wenzake. (Gazzetta dello Sport, in Italian)

Rais wa klabu ya Napoli Aurelio de Laurentiis amepokea Euro milioni 560 kwa ajili ya Ligi ya klabu ya Serie A kutoka Qatar huku mashabiki wakipinga na wachezaji wakigoma . (Mail)

Nemanja Matic anataka kuondoka Manchester United, ikiwezekana mwezi Januari, huku kiungo huyo wa kati Mserbia mwenye umri wa miaka 31 akitarajiwa kwenda Italia. (telegraph)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino huenda akafutwa kazi baada ya Spurs kushindwa na West Ham baada ya kipindi cha mapumziko cha kimataifa. (Telegraph)
Pep Guardiola, ambaye alikuwa kocha wa Bayern
Munich kwa misimu mitatu kabla ya kuwasili Manchester City, anaweza
kurejea katika Bavaria wakati Niko Kovac anasemekana kuondoka katika
timu hiyo. (The Athletic, subscription required) Fiorentina wamefanya mazungumzo na meneja wa zamani wa Inter Milan Luciano Spalletti huku wakionyesha kuwa wamemchoka Vincenzo Montella. (Football Italia)
Arsenal wanamfanyia majaribio mchezaji wa safu ya
kati wa klabu ya Colorado Rapids Cole Bassett na kijana huyo
Mmarekani mwenye umri wa miaka 18 anaweza kujiunga na Gunners mwezi
Januari. (Sun)Wolves wameafiki mkataba wa kumleta kikosini Mholanzi Nigel Lonwijk mwenye umri wa miaka 17 kutoka klabu ya PSV Eindhoven anayecheza katika safu ya kati ifikapo mwezi Januari kwa pauni £170,000. (ED via Birmingham Live)
Lyon wanasaka mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema, mwenye umri wa miaka 31, kumalizia mchezo kule alikouanzia katika klabu hiyo ya Ufaransa. (Mundo Deportivo, in Spanish)
0 comments:
Post a Comment