Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuhusiana na baadhi ya madai ya wachezaji kujihusisha na ushirikina.
ahera amefunguka hayo wakati akihojiwa na gazeti la Championi kufuatia kuwepo kwa tetesi hizo kuwa ushirikina umekuwa ukichukua nafasi ndani ya kikosi kwa baadhi ya wachezaji kwa kufunguka yafuatayo:
Swali lilikuwa hivi: UNAZUNGUMZIAJE MADAI YA WACHEZAJI WAKIKIMBIA KUCHEZA NAFASI YA JUMA ABDUL KWA KUWA WANAUMIA WAKIHUSISHA NA USHIRIKINA?
“Ni kweli alicheza Mapinduzi aliumia lakini sikuweza kumtumia Juma Abdul kwa kuwa alichelewa kwenye maandalizi ya msimu kutokana na matatizo yake na uongozi akiwa na Dante.
“Sasa wakati anakuja Morogoro sisi tulikuwa tumeshamaliza maandalizi yeye ndiyo akawa amekuja lakini hakuwa anacheza kwa kuwa hakuwa fiti kabisa tofauti na wenzake lakini tulivyokuwa Mwanza ambapo nilipanga kuanza kumtumia ndiyo akapatwa na msiba wa mama yake, akaondoka.
“Nilimchukua katika safari ya Zambia kwa ajili ya kukamilisha idadi lakini siyo kucheza kwa kuwa bado hakuwa sawa na siyo kweli kwamba wachezaji walikuwa wakiogopa kucheza kwenye nafasi hiyo,” anamalizia Zahera.

0 comments:
Post a Comment