
Manchester United wamefufua tena juhudi za kumsajili nyota wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 25. (Goal.com)
Barcelona
iko mbioni kumsaka Dani Olmo wa Dinamo Zagreb licha ya nyota huyo
kung'ang'aniwa na Chelsea na Manchester United ambapo tayari wamefanya
mazungumzo na klabu hiyo kuhusu usajili wa mshambuliaji huyo wa
Uhispania wa miaka 21. (Goal.com)Arsenal wamewasilisha ombi rasmi kwa Bayern Munich kuhusu usajili wa beki wa wa Ujerumani Jerome Boateng, 31. (Footmercato - in French)
Chelsea imeanza mkakati wa kumsaka mshambuliaji wa Inter Milan na Brazil Gabriel Barbosa, 23, mwezi huuwa Januari Frank Lampard akipania kumsajili mshambuliaji mpya. (Daily Express)
Kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard, 27, ameungana na ajenti Mino Raiola, baada ya tetesi kuzuka kwamba huenda akaondoka Old Trafford. (Mail)
Watford imeungana na Everton katika kinyang'anyiro cha usajili wa mshambuliaji wa Carlisle wa miaka 17- Muingereza Jarrad Branthwaite. (Watford Observer)
Mashabiki wa Liverpool wamevutiwa na mpango wa usajili wa Ousmane Dembele, baada ya mshambuliaji huyo wa miaka 22- wa Barcelona na Ufaransa kubonyeza Like, picha inayomonesha akiwa amevalia jezi nyekundu nstagram . (Daily Express)
Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anawasaka wambuliaji wawili mwezi huu wa Januari dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa. (South London Press)
Beki wa Burnley Ben Gibson, 26, ananyatiwa na klabu ya Eintracht Frankfurt na Cologne nchini Ujerumani. (Daily Mail)

Tetesi Bora Jumapili
Man United wako tayari kutoa kiasi cha Pauni million 45 ili kumnasa nyota wa Leicester City James Maddson na watamtoa Jesse Lingard ili kuweza kufanikisha usajili huo.West ham watapigana vikumbo na Man City katika kuwania saini ya beki kisiki wa Napoli Kalidou Koulibali. (Sunday Express)
Juventus wamefanya mazungumzo ya awali na Chelsea ili kuangalia uwezokano wa kumsajili beki wa kushoto wa timu hiyo mbrazil Emerson.
0 comments:
Post a Comment