GARY
Neville, mchezaji wa zamani wa Manchester United amesema kuwa anaamini
nyota wa Liverpool, Mohamed Salah anaweza kujiunga na timu za Barcelona
ama Real Madrid wakati ujao.
Neville
amesema kuwa anatambua uwezo wa mshambuliaji huyo ni mkubwa na huenda
mashabiki wake wengi watafurahi kumuona akipata changamoto mpya akiwa
sehemu nyingini.
Salah
raia wa Misri, ametupia jumla ya mabao 90 kwenye mechi 140 ambazo
amecheza mpaka sasa akiwa na Liverpool ambayo alijiunga nayo mwaka 2017
na ametwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa akiwa na timu hiyo.
"Sio
kitu chepesi kumpata mchezaji kama Salah na niliwahi kusema miezi 18
iliyopita kuwa Salah yupo njiani kuondoka ndani ya Liverpool.
"Ninaamini
itakuwa ngumu kutokana na mashabiki wake wa Liverpool kupenda kumuona
pale ila wapo wengine ambao watapenda kumuona sehemu nyingine kutokana
na thamani yake aliyojiwekea,".

0 comments:
Post a Comment