Barcelona inampango wa kuuza haki ya jina
la uwanja Nou Camp kwa muda wa mwaka mmoja ili kupata fedha zitakazoweza
kuwasaidia katika vita vya kiuchumi dhidi ya janga la virusi vya
corona.

Kuuzwa kwa jina hilo Nou Camp, kutaweza kushuhudiwa moja kati ya viwanja vyenye historia kubwa katika mchezo wa soka duniani vikianza kupoteza tamaduni zake.
Bodi ya utendaji ndani
ya Barcelona, Jumanne imesema klabu itakusanya fedha zote zitakazotokana
na mauzo ya haki ya jina Nou Camp ili kusaidia vita dhidi ya virusi vya
corona.
Nou Camp ni moja ya uwanja
mkubwa kabisa barani Ulaya, wenye viti zaidi ya 99,000 na haukuwahi kuwa
na mdhamini tangu kufunguliwa kwake mwaka 1957.
Klabu
itasubiri kuuza haki ya jina la uwanja huo kwa mara ya kwanza ifikapo
msimu wa mwaka 2023-24. Katika muda huo Barcelona inaamini itaweza
kuingiza kitita cha fedha paundi milioni 264.
Baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo ya Barcelona wanaamini kuwa huo ndiyo utakuwa mwanzo wa kupotea kwa tamaduni za uwanja wao.
Makamu
wa Rais wa Barcelona amesema ”Tunataka kuwatumia ujumbe kwa wote. Kwa
mara ya kwanza mtu atakuwa na nafasi ya kuweka jina lake Nou Camp.”
0 comments:
Post a Comment