GWIJI
wa Manchester United, Paul Scholes, amesifu mchango ulioletwa na Bruno
Fernandes klabuni hapo, akisema raia huyo wa Ureno amekuja na kitu
kilichokosekana kwa muda mrefu United.
Mara
baada ya kujiunga akitokea Sportling Januari, Fernandes ameisaidia
United kucheza mechi 11 mfululizo bila kupoteza kabla ya ligi
kusimamishwa kutokana na Virusi vya Corona.
Katika
mechi tisa za michuano yote akiwa na United, nyota huyo mwenye miaka
25, amefunga mabao matatu na asisti nne akikisaidia kikosi cha Ole
Gunnar Solskjaer kuwa na muunganiko mzuri kutokea nyuma kwenda kwenye
ushambuliaji.
Scholes
amesema Mreno huyo ameongeza kitu kwenye safu ya kiungo ya United,
ingawa anakiri kwamba bado hana uhakika ni mfumo gani unamfanya acheze
vizuri zaidi.
“Haonekani
kama ni kiungo wa kati kwangu mimi, namuona kama namba 10 wa kutoka na
kuingia, daima anageuka na ni kiunganishi ambacho United ilikihitaji
sana,” alisema Scholes.
“Walikosa
ubora huo kwenye kiungo na tangu alipokuja, ameuleta. Anaweza kuwalisha
mipira wachezaji, anaweza kupiga mashuti na anaonekana ni kiongozi wa
kweli pia. United ilikosa mtu wa namna hiyo.
“Yupo kama Eric Cantona au Teddy Sheringham – anaweza kuwapita wapinzani pia.”
0 comments:
Post a Comment