Monday, April 13, 2020



RONALDO Luis Nazario de Lima, nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil ana umri wa miaka 43.

Ni miongoni mwa nyota ambao wanatajwa kuwa bora kwa muda wote zama zake wakati akikipiga akiwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, spidi na kufunga mabao kwa nafasi yake ya ushambuliaji.
Alitikisa zaidi  kwenye Kombe la dunia mwaka 1998, 2000 kutokana na ubora wake kazi yake ilitukuka zaidi akiwa na klabu za Inter, Ac Milan, Barca na Real Madrid.
Mwaka 1997 na 2002 alikuwa mchezaji bora wa dunia alitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa  mwaka 1997/98 akiwa na Inter na makombe mengine kibao.

Alishastaafu kitambo kwenye ulimwengu wa soka na anamiliki klabu ya Real Valladolid. Kwenye maisha yake ya soka amecheza jumla ya mechi 343 na ametupia mabao 247.

0 comments:

Post a Comment