
Winga wa Borussia
Dortmund na England Jadon Sancho, 20, hana mpango wa kujiunga na
Chelsea, hatua ambayo inaiweka Manchester United katika nafasi nzuri ya
kupata saini yake japo Real Madrid pia wanapigiwa upatu kumsajili nyota
huyo. (Diario Madridista, in Spanish)
Barcelona wanatazamiwa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham mfaransa Tanguy Ndombele, 23. (Star)Everton wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsaka mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez. Manchester United na Juventuspia wanamnyatia nyota huyo wa miaka 28. (Express)

Roma haijakubali kufikia bei ya Arsenal ya £22m kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan. Muarmenia huyo wa miaka 31, yupo klabu hiyo ya Italia inayoshiriki Ligi ya Serie A kwa mkopo wa msimu mzima. (Calciomercato, via Star)

Hatahivyo, naibu rais wa Inter Milan Javier Zanetti anaamini Martinez atasalia katika klabu hiyo. (ESPN)
Beki wa Inter Milan na Uruguay Diego Godin huenda akahamia Ligi ya Premia msimu huu wa joto. Manchester United na Tottenham pia wanamtaka mchezaji huyo wa miaka 34. (Tuttosport, in Italian)

Mkufunzi wa Southampton Ralph Hasenhuttl amekubali kusalia katika klabu hiyo kwa miaka mitatu. (Sun)

Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice amesema angelipendelea kucheza tena na mwezake wa Chelsea Mason Mount. Wawili hao, ambao wote wana miaka 21, walikuwa pamoja katika chuo cha mafunzo ya soka cha Chelsea. (Copa90)

0 comments:
Post a Comment