
Imependekezwa pia uwanja wa Wembley ndio utatumika kama “neutral-ground” na kwa siku zaidi ya michezo minne ifanyike. Vilabu vinataka kumaliza msimu ili kuepuka athara kutoka kwenye kampuni za Televisheni – ambapo bila hivyo vilabu vinaweza kulipa fedha nyingi.
Chanzo kimeeleza kuwa ” Hadi Kufikia mwezi Juni au Julai vilabu vitakuwa vikicheza michezo yao bila mshabiki ingawa itakuwa ikiruka live kupitia runinga” Itabidi kucheza michezo minne kwa siku katika uwanja wa Wembley ili kuimaliza kwani vilabu vingine vina michezo takribani tisa watafanya hivyo ili kumaliza msimu”

Hadi sasa, hakuna tarehe maalumu ya kurudi iliyowekwa ambayo itakuwa rasmu kwa kureje Ligi Kuu, ingawa katika taifa hilo bado watu hawatakiwa kutoka nje kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
0 comments:
Post a Comment