KLABU
ya ES Setif inayoshiriki Ligi Kuu ya Algeria imeweka ofa mezani kwa
ajili ya kumnasa mshambuliaji wa Yanga, David Molinga ‘Falcao’.
Nyota
huyo ambaye ni mpachika mabao namba moja ndani ya Yanga amekuwa hana
nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa
kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona.
Nyota
huyo kwa sasa anafikiria kusepa ndani ya kikosi hicho kutokana na
kukosa namba ya kudumu tofauti na zama za Mwinyi Zahera ambapo alikuwa
na uhakika wa kutumia dakika 90 uwanjani.
Kocha
Mkuu wa Yanga, Luc Eymael alisema kuwa kinachomshinda Molinga uwanjani
ni kushindwa kutulia sehemu moja huku akisema kuwa ishu ya kuondoka
ndani ya Yanga lipo chini ya viongozi.
"Miongoni
mwa wachezaji wazuri lakini anashindwa kutulia sehemu moja muda mwingi
anazungukazunguka, akipata nafasi atakuja kuwa vizuri iwapo kuna masuala
ya mchezaji kuondoka hayo yanahusu utawala.
0 comments:
Post a Comment