HATIMAYE
Ronaldinho nyota wa zamani wa Klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya
Brazil na kaka yake Assis wamepata dhamana na kutoka gerezani nchini
Paraguay baada ya kukaa huko kwa siku 32.
Ronaldinho
na Kaka yake wamepata dhamana kwa dola milioni 1.6 (Tsh Bilioni 3.7)
baada ya awali kukataliwa dhamana nyepesi kwa hofu wangeweza kutoroka.
Pamoja
na kupata dhamana hiyo jaji Gustavo Amarilla ameamuru wawili hao
kutolewa gerezani na kwenda kuishi katika nyumba/hotel katika mji wa
Asuncion wakiwa chini ya uangalizi maalum.
Ronaldinho
na Assis walikamatwa na Polisi nchini Paraguay kwa tuhuma za kuingia
nchini humo na Passport feki za Paraguay ambazo zinawaonesha wao kama
raia wa nchi hiyo wakati ni raia wa Brazil.
0 comments:
Post a Comment