OLE
Gunnar Solskajer, Kocha Mkuu wa Manchester United,amesema kuwa kuibuka
kwa Virusi vya Corona kunaweza kuwa na faida kwao kuelekea kwenye
dirisha la usajili.
Kwa
sasa dunia nzima ipo kwenye janga la kupambana na Virusi vya Corona
ambapo klabu nyingi zinapambana kupunguza matumizi ili kuweza kujiepusha
na anguko la kiuchumi.
Solskjaer,
amedai kuwa, baadhi ya klabu zitalazimika kuuza wachezaji kutokana na
kuanguka kiuchumi, hivyo wao kama Man United, wataitumia fursa hii
kupata wachezaji wa kiwango cha juu.
Miongoni
mwa wachezaji ambao wanatajwa kuwindwa na United ni pamoja na Jadon
Sancho, Jack Grealish, Jude Bellingham, Willian na Icard.
0 comments:
Post a Comment