
Klabu ya Real
Madrid imeahirisha mipango yake ya kumsajili mshambuliaji nyota wa
Ufaransa Kylian Mbappe, 21, kutoka Paris Saint-Germain mpaka 2021
kutokana na janga la virusi vya corona. (AS)
Klabu za Arsenal,
Chelsea na Celtic wanamuwania mshambuliaji kinda wa Middlesbrough na
timu ya taifa ya chini ya miaka 17 ya Jamhuri ya Ireland Calum Kavanagh,
16. (Sun)Liverpool imejiunga na msururu wa klabu zinazovutiwa na kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Lille ya Ufaransa Boubakary Soumare, 21. Klabu za Real Madrid, Manchester United, Chelsea na Newcastle pia zinamuwania mchezaji huyo. (Sport)

Klabu ya AC Milan imetuma maombi ya kutaka kumsajili kiungo wa Manchester City David Silva, 34. Kiungo huyo raia wa Uhispania anamaliza mkataba wake na City mwishoni mwa msimu. (Corriere Dello Sport - in Italian)
AC Milan pia wanaandaa pauni milioni 35 ili kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Uruguay Lucas Torreira, 24. (Corriere Dello Sport - in Italian)

Winga Yannick Bolasie, 30, anatarajiwa kurejea Everton kutoka Sporting Lisbon mwishoni mwa msimu kulingana na wakala wake. lakini miamba hiyo ya Ureno haitaki kumsajili moja kwa moja. (Record - in Portuguese)

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE

Barcelona wanataka
kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, kutoka klabu
ya Inter Milan lakini wanakabiliana na ushindani mkali kutoka kwa Real
Madrid na Manchester City. (Marca)
Klabu ya Wolves haitamuuza
Adama Troare, 24, kwa dau lolote chini ya pauni milioni 70 huku winga
huyo akihusishwa na mipango ya kuhamia Liverpool. (Football Insider)Arsenal wanalenga kumsajili beki wa Athletic Bilbao Unai Nunez, 23, kama kipaumbele chao kwa usajili wa majira ya kiangazi. Beki huyo wa Uhispania ana kifungu cha mkataba kinachoelekeza kuuzwa kwa euro milioni 30. (La Razon - in Spanish)

Liverpool, Manchester City na Manchester United wote wameonesha nia ya kumsajili winga wa Uhispania na Valencia Ferran Torres, 20. (Goal)
Kiungo wa Manchester United Jesse Lingard, 27, hana mpango wa kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu. Kiungo huyo anahusishwa na uhamisho kuelekea Arsenal na Everton. (Metro)

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, amefanya mazungumzo ya awali juu ya kuongeza mkataba katika klabu ya Chelsea. (Football.London)
Chelsea pia inajipanga kushindana na Arsenal katika mbio za kumsajili beki yaw a Ujerumani Jerome Boateng, ambaye anakaribia kuingia katika miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake na klabu ya Bayern Munich. (Mail)
TETESI ZA SOKA JUMATATU

Mshambuliaji wa
Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England Jadon Sancho, 20, amekataa
uhamisho wa kuelekea Manchester United mwisho wa msimu huu iwapo
watashindwa kufuzu katika michuano ya klabu bingwa (Sun)
Real Madrid inataka kumsaini mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane mwenye umri wa miaka 26. (Sport)
Leicester, Newcastle, Crystal Palace na Aston Villa wana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Rangers na Colombia Alfredo Morelos, 23. (Talksport)
- Tetesi za soka Ulaya Jumapili 05.04.2020
- 'Ni haki yao Liverpool wapewe ubingwa'
- Wachezaji wachanga wenye thamani kubwa duniani watangazwa

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa sasa anahudumu kwa mkopo katika klabu ya Inter Milan kutoka Man United. (Sport Witness)
Kiungo wa kati wa Manchester City na Uhispania David Silva, 34, huenda akapatiwa mechi ya mwisho ya kumuaga katika uwanja wa Etihad mwisho wa msimu iwapo mlipuko wa coronavirus utamzuia kuwaaga mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuichezea klabu hiyo kwa miaka 10 kitu ambacho kimemsaidia kushinda taji la ligi kuu mara. (Mail)

Leicester, Tottenham na Everton wote wana hamu ya kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 Baptiste Santamaria, ambaye anaichezea klabu ya Angers katika ligi ya daraja la kwanza ya Ufaransa. (Express)
Klabu za ligi ya Premia zimenunua vifaa vyao vya kupima virusi vya corona huku kukiwa na hofu kwamba mechi zitachezwa bila mashabiki. (Star)
Beki wa Uholanzi na Manchester United Timothy Fosu-Mensah, 22, anakabiliwa na hali ya switofahamu katika klabu hiyo huku mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer akifikiria iwapo anaweza kumuongezea mwaka mmoja katika kandarasi yake (Mirror)
0 comments:
Post a Comment