
Everton
imewasilisha ombi la £40m kumsaini kiungo wa kati wa Napoli, Allan, 29,
lakini klabu hiyo inataka dau la £60m kumuuza raia huyo wa Brazil. (Il
Mattino - in Italian)
The Toffees pia wamewasilisha ombi la $25m
kwa Barcelona kumnunua beki wa Ufaransa Jean -Claire Todibo ,20, ambaye
kwa sasa anahudumu kwa mkopo katika klabu ya Schalke nchini Ujerumani.
(Mail)
Mmiliki wa Bournemouth Maxim Demin karibu aiuze klabu hiyo kwa mfanyabiashara wa Saudia mnamo mwezi Januari , kabla ya makubaliano hayo kugonga mwamba kuhusiana na thamani ya klabu hiyo. (90min)

Chelsea imeamua kutotumia kifungu chake cha sheria dhidi ya winga wa Ivory Coast Jeremie Boga ,20, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda kuichezea klabu ya Napoli. (Guardian)

Paris St-Germain inafanya mazungumzo na Arsenal katika jaribio la kumsaini mashambuliaji wa klabu hiyo Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kwa£34m. (Todofichajes)
Tetesi za Soka Jumatatu
Mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 32, huenda akarudi katika ligi ya premia baada ya uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Chelsea - Newcastle na Wolves zote zinamwania. (Express)
Barcelona iko tayari kumuuza mashambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 23, kwa dau la £37m. Klabu hiyo ya Uhispania ililipa £137m kumnunua raia huyo wa Ufaransa miaka mitatu iliopita lakini ameanzishwa mara tano pekee kufuatia msururu wa majeraha. (Mirror)

0 comments:
Post a Comment