Mechi ya mahasimu Real Betis na Sevilla inatarajiwa kufungua
dimba la kurejea kwa msimu wa Ligi Kuu ya Kandanda ya Uhispania mnamo
Juni 11.
Kama ilivyo kwa
ligi nyengine ulimwenguni, ligi hiyo maarufu kama La Liga ililazimika
kusimamishwa mwezi Machi kwa muda usiojulikana kutokana na mlipuko wa
virusi vya corona. Ligi hiyo pia itarejea kwa michezo ambayo
haitahudhuriwa na mashabiki uwanjani kama ilivyo kwa Ujermuani.
Mkuu
wa La Liga Javier Tebas ameiambia runinga moja nchini Uhispania kuwa
mechi hiyo "itakuwa ni tuzo maalumu kwa wote waliofariki".
Hata
hivyo, Tebas amewaonya wachezaji wawe "waangalifu na matendo yao" baada
ya wachezaji wanne wa Sevilla kuomba radhi kwa kuvunja masharti ya
kujiteng katika jamii.
Wachezaji hao Ever Banega, Lucas Ocampos,
Franco Vazquez na Luuk de Jong walipigwa picha katika mjumuiko wa
sherehe mwishoni mwa wiki.
Uhispania umelegeza masharti ya marufuku ya watu kutokutoka nje, lakini mikusanyiko ya Zaidi ya ya watu 10 badoo ni marufuku.
"Wachezaji ni mfano kwa jamii, na wanapaswa kuwa makini na matendo yao," ameeleza Tebas.
"Nawataka wachezaji wote kutokuwa kama hivi. Inatubidi tuwe makini kwa kuwa ajira za watu wengi zipo hatarini."
Siku
ya Jumamosi, Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez alitoa ruhusa kwa
ligi za juu za kandanda kurejea nchini humo kuanzia Juni 8.
Wachezaji
wa La Liga walianza mazoezi katika makundi ya wachezaji wasiozidi 10
wiki iliyopita. Tabias anaeleza kuwa lengo sasa ni kurejesha mazoezi
kamili.
"Kwa sasa hilo ndilo lengo letu, na tukishafanikisha hilo
tutaweza kuirejesha ligi. Shabaha yetu ni kutangaza tratiba ya
mizunguko ya mechi wiki ijayo."
"Tangazo la serikali lilitushtua, laikni linaonesha ni kwa namna gani mpira wa kulipwa ni muhimu sana kwa nchi hii."
Miamba Barcelona inaongoza ligi hiyo kwa alama mbili mbele ya Real Madrid huku kukiwa na mechi 11 ili kukamilisha msimu.
Wachezaji
wa ligi mbili madaraja ya juu waliweza kurejea katika mazoezi binafsi
mapema mwezi huu wa Mei baada ya kufanyiwa vipimo vya corona.
Wachezaji
watano walikutwa na virusi katika ligi hizo mbili na wakajitenga
karantini kabla ya ruhusa ya mazoezi ya makundi kuanza Mei 18.
Wakati
huo huo, Ligi Kuu ya Ureno inatarajiwa kurejea Juni kwa michezo miwili.
Klabu ya Portimonense itaminyana na Gil Vicente huku Famalicao
ikiwakaribisha vinara Porto.
Porto wapo kileleni kwa tofauti ya alama moja dhidi ya mahasimu wao Benfica huku mechi 10 zikisalia kabla msimu ufikie tamati.
0 comments:
Post a Comment