Thursday, September 10, 2020


NYOTA wa Manchester City, Kevin De Bruyne ameshinda tuzo ya kwanza kabisa ya Mchezaji Bora wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) usiku wa jana.
Mbelgiji huyo amefikia rekodi ya Mfaransa Thierry Henry katika Ligi Kuu ya England, kutoa pasi za mabao 20 kwa msimu mmoja, Man City ikimaliza nafasi ya pili nyuma ya mabingwa, Liverpool.
De Bruyne amemshinda mchezaji mwenzake, Raheem Sterling, ambaye amekuwa mchezaji wa kwanza wa Man City kumaliza msimu na mabao mengi zaidi ya Sergio Aguero tangu Muargentina huyo asajiliwe mwaka 2011.
Kevin De Bruyne ameshinda tuzo ya kwanza kabisa ya Mchezaji Bora wa PFA usiku wa jana 

Nyota wanne wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold – aliyeshinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa PFA – Jordan Henderson, Virgil Van Dijk na Sadio Mane pa waliingia fainali.
Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool ameingiza wachezaji watano kwenye kikosi cha Msimu cha PFA, Manchester City na Leicester City zikiingiza wawili kila timu – wakati  wengine ni Nick Pope na Pierre-Emerick Aubameyang wa Arsenal.

 

0 comments:

Post a Comment