BEKI wa Mbao FC, Asante Kwasi amesema kwamba amekataa kujiunga na Singida United ili kusubiri uwezekano wa kusajiliwa na Azam kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Akizungumza na blog hii, Kwasi alisema kwamba kwa sasa yeye ni mchezaji huru hivyo yupo tayari kutumikia timu yoyote kikubwa anaangalia maslah.
Kwasi ambaye ni mchezaji huru kwa sasa baada ya kumaliza mkataba wake Mbao FC, alisema kocha wa Singida United, Hans van der Pluijm amempa ofa ya kujiunga na timu yake iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, lakini amekataa.
"Ninaipenda Azam kutokana na inavyoendeshwa kisasa, natamani siku moja nichezee timu hiyo, kama timu nyingine zitakuja na dau nzuri basi sina budi kusaini," alisema raia huyo wa Ghana.
Kwasi amekuwa na msimu mzuri Mbao FC akiiwezesha kubaki Ligi Kuu katika msimu wake wa kwanza baada ya kupanda na pia kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) ambako walifungwa na Simba 2-1.
0 comments:
Post a Comment