by alanus
Kikosi cha timu ya wasichana ya soka
ya Shule ya Sekondari ya Makongo, kimeanza kujifua kwa ajili ya kujiweka sawa
kwa michuano ya Shule za Sekondari maarufu kama Ummiseta.
Kikosi hicho, leo kimefanya mazoezi
kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi hayo.
Walianza na mazoezi ya kukimbia
ambayo yalionekana kuwa magumu lakini kocha wao alihimiza kuhakikisha
wanamaliza.
Baada ya hapo waliendelea na mazoezi
mengine ikiwa ni pamoja na "kuupiga" hali inayoonyesha wako vizuri.
0 comments:
Post a Comment