MECHI ZA MWISHO
Jumamosi Mei 20
Azam FC v Kagera Sugar
Maji Maji FC v Mbeya City
Simba v Mwadui FC
Mbao FC v Yanga
Stand United v Ruvu Shooting
Mtibwa Sugar v Toto Africans
Tanzania Prisons v African Lyon
Ndanda FC v JKT Ruvu
+++++++++++++++++++++
YANGA, ambao ni Mabingwa Watetezi wa VPL, Ligi Kuu Vodacom Leo wako huko CCM Kirumba Jijini Mwanza kuhitimisha utetezi wa Ubingwa wao wakihitaji Pointi 1 tu katika Mechi hii ya mwisho ya Msimu wa Ligi.
Lakini, kwa hali ilivyo sasa, hata Yanga, ambao wako Pointi 3 mbele ya Simba, akifungwa Mechi hii bado Simba ana kazi mbili kubwa ili kutwaa Ubingwa na hizo ni kwanza waifunge Mwadui FC na pili ushindi huo uwe Bao
Ukiondoa hayo na ukichukua makandokando, Simba Juzi ilithibitisha kuwa FIFA imeshapokea Rufaa yao ya kupinga kupokwa Pointi 3 ilizopewa na Kamati ya Masaa 72 ya TFF baada kufungwa na Kagera Sugar na wao kudai alichezeshwa Mchezaji aliekuwa na Kadi za Njano 3.
Hili litaifanya Yanga Leo kusaka ushindi kwa udi na uvumba ili waifunge Mbao FC ili kuondoa mzizi wa fitina endapo FIFA itaipa Simba Pointi 3 kwani ushindi huo utafuta kabisa matumaini hayo ya Simba ya kucheza 'Mpira Mezani'.
Huu utakuwa Ubingwa wa Yanga wa 3 mfululizo na wa 5 ndani ya Miaka 6 na wa 26 katika Historia yao ya Miaka 26 wakishika Rekodi kupita Timu yeyote.
Kwa kutwaa Ubingwa mara 3 mfululizo, TFF italazimika kuwapa Yanga Kombe la Ubingwa moja kwa moja liwe lao la kudumu na Msimu ujao kutoa Kombe jipya kabisa.
Hilo limethibitishwa na TFF.
Hii itakuwa ni mara ya 3 kwa Yanga kuutwaa Ubingwa mara 3 mfululizo tangu Mwaka 1965 ambapo Mfumo rasmi wa Ligi ulianzishwa.
Yanga ilitwaa Ubingwa mara 3 mfululizo kwenye Miaka ya 1991- 1993, 1996- 1998 na sasa kipindi hiki cha 2014 – 2017.
Mbali ya sakata hili la Ubingwa pia ipo vita kubwa ya Timu zipi 2 zitaungana na JKT Ruvu kushushwa Daraja.
Timu ambazo zipo hatarini ni Toto Africans, Ndanda FC, Mbao FC, African Lyon, Maji Maji FC na Mbeya City ambao kidogo Tofauti ya Magoli yao Bora inaweza kuwalinda.
0 comments:
Post a Comment