
Baada
kuenea kwa taarifa za Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba kupigwa
chini, mwenyewe ameibuka na kueleza kinachoendelea ndani ya klabu hiyo.
Kawemba
ameeleza kuwa bado anaendelea na majukumu yake ndani ya klabu hiyo,
lakini mkataba wake unaelekea ukingoni huku akiwashangaa wanaoeneza
taarifa hizo.
“Unajua
watu wanasema mengi, lakini kiukweli hakuna mtu aliyenifukuza Azam, kwa
sababu hivi sasa natoka zangu ofisini naelekea Chamazi, sasa
inawezekanaje nifukuzwe halafu bado niendelee kuwepo katika ofisi zao?
Nasikia mengi maana hata nilivyokuwa TFF mengi yaliongelewa, hivyo
hakuna kipya.
“Lakini
pia wanatakiwa kujua kwamba nafanya kazi kwa mkataba ambao unaelekea
ukingoni na utamalizika mwezi huu na hiyo ni kawaida kwa mtu yeyote
mkataba unapoisha lazima aondoke au abaki, siyo kwangu tu, na tupo
katika mazungumzo, kama yakienda vizuri nitaongeza mkataba,” alisema Kawemba, jana.
0 comments:
Post a Comment