by alanus
Robert Lewandowski alikasirishwa na wachezaji wenzake kutompa sapiti mwishoni mwa msimu akiwania ufungaji bora wa BUndesliga PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KLABU
ya Bayern Munich imewaonya wapinzani wanaotaka kumchukua mshambuliaji
wao Robert Lewandowski, kwamba wataadhibiwa na Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA).
Chelsea
na Manchester United zote zimeripotiwa kumfiatilia mwanasoka huyo wa
kimataifa wa Poland huku ikiamini na tayari zimekwishawasiliana na
wakala wa Lewandowski, ambaye amesema mteja wake hakuwa na furaha.
Taarifa
ya klabu hiyo imesema: "Mkataba wa Lewandowski unamalizika mwaka 2021,
alisaini si muda mrefu uliopita. Lewandowski hataki kuondoka Bayern.
Hakuna mazungumzo na klabu nyingine na haiwezi kuwa yoyote. Ikiwa klabu
nyingine zinazungumza na mchezaji mwenye mkataba mrefu zinajihatarisha
kuadhibiwa na FIFA," imesema taarifa hiyo.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 28 inafahamika hana furaha Bayern na wakala
wake, Maik Barthel amesema kwamba uongozi na wachezaji wenzake hawakumpa
sapoti ya kutosha mwishoni mwa msimu wakati anapigania ufungaji bora na
alicheza licha ya kuwa na maumivu ya bega.
Lewandowski
aliongeze mkataba Desemba mwaka jana hadi mwaka 2021 na mbali na
Chelsea na Man United, klabu nyingine inayotajwa kumuhitaji ni Real
Madrid.

0 comments:
Post a Comment