Details
Created: Thursday, 22 June 2017 05:21
>LEO CAMEROON-AUSTRALIA & GERMANY-CHILE!
JANA
Mexico walitoka nyuma na kuifyeka New Zealana Bao 2-1 kati Mechi yao ya Pili ya
Kundi A la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara ndani ya Fisht Stadium Jijini
Sochi huko Nchini Russia.
Mapema
Jana, katika Mechi nyingine ya Kundi A, Portugal iliwafunga Wenyeji Russia 1-0
kwa Bao la Cristiano Ronaldo.
Hizo
zilikuwa ni Mechi za Pili kwa kila Timu katika Kundi A na kuzifanya Mexico na
Portugal zifungane uongozini zikiwa na Pointi 4 kila moja lakini Mexico wako
juu kwa Mabao, Watatu ni Russia wenye Pointi 3 na mkiani ni New Zealand ambao
tayari washaaga Mashindano.
Timu 2 za
juu za kila Kundi zitasonga Nusu Fainali.
New
Zealand walitangulia kufunga katika Dakika ya 42 kwa Bao la Chris Wood,
anaecheza England na Klabu ya Leeds United, lakini Mexico, ambao Jana Kocha wao
Juan Carlos Osoria alibadili Wachezaji 8 toka kile Kikosi kilichotoka Sare 2-2
na Portugal akiwemo Javier Hernandez ‘Chicharito’, walijibu Kipindi cha Pili na
kufunga Bao 2.
Bao za
Mexico zilifungwa na Raul Jimenez na Oribe Peralta.
++++++++++++++++
++++++++++++++++
Mechi hii ilikumbwa na mzozo mwishoni wakati Diego Reyes Nahodha wa
Mexico alipomvuta Michael Boxall na kisha Hector Herrera kuingilia nah apo Ryan
Thomas wa New Zealand kuvamia sakata hilo.
Refa
Bakary Gassama kutoka Gambia akaitisha msaada wa VAR, Video Assistant Referee.
Na baadae kutoka Kadi za Njano 3 kwa Reyes, Herrera na Boxall.
Leo zipo
Mechi 2 za Kundi B ambazo zitakuwa Mechi za Pili kwa kila Timu, wakati Cameroon
wataanza na Australia na kisha Mabingwa wa Dunia Germany kucheza na Chile.
VIKOSI VILIVYOANZA:
NEW ZEALAND (Mfumo 5-3-2): Marinovic; Ingham, Boxall, Durante, Smith, Wynne; McGlinchey,
Rojas, Thomas; Lewis, Wood.
Akiba:
Brotherton, Tzimopoulos, Tuiloma, Barbarouses, Smeltz, Moss, Patterson, Doyle,
Colvey, Rufer, Roux, Williams.
MEXICO (Mfumo 3-5-2): Talavera; Salcedo, Araujo, Alanis; Damm, D. Reyes, G. Dos
Santos, Fabian, Aquino; Jimenez, Peralta
Akiba:
Cota, Marquez, J. Dos Santos, Layun, Vela, Ochoa, Hernandez, Moreno, Herrera,
Guardado, R. Reyes, Lozano
REFA: Bakary Gassama [Gambia]
++++++++++++++++
FIFA KOMBE LA MABARA
Ratiba/Matokeo:
Hatua ya Kwanza
Jumamosi Juni 17
KUNDI A
Russia 2 New Zealand 0
Jumapili Juni 18
KUNDI A
Kazan Arena, Kazan
Portugal 2 Mexico 2
KUNDI B
Spartak Stadium, Moscow
Cameroon 0 Chile 2
Jumatatu Juni 19
KUNDI B
Australia 2 Germany 3
Jumatano Juni 21
KUNDI A
Russia 0 Portugal 1
Mexico 2 New Zealand 1
Alhamisi Juni 22
KUNDI B
Saint Petersburg Stadium, Saint
Petersburg
1800 Cameroon v Australia
Kazan Arena, Kazan
2100 Germany v Chile
Jumamosi Juni 24
KUNDI A
Kazan Arena, Kazan
1800 Mexico v Russia
Saint Petersburg Stadium, Saint
Petersburg
1800 New Zealand v Portugal
Jumapili Juni 25
KUNDI B
Fisht Stadium, Sochi
1800 Germany v Cameroon
Spartak Stadium, Moscow
1800 Chile v Australia
Hatua ya Pili
Nusu Fainali
Jumatano Juni 28
Kazan Arena, Kazan
2100 Mshindi Kundi A v Mshindi wa
Pili Kundi B [NF1]
Alhamisi Juni 29
Fisht Stadium, Sochi
2100 Mshindi Kundi B v Mshindi wa
Pili Kundi A [NF2]
Mshindi wa 3
Jumapili Julai 2
Spartak Stadium, Moscow
1500 Atakaefungwa NF1 v Atakaefungwa
NF2
FAINALI
Jumapili Julai 2
Saint Petersburg Stadium, Saint
Petersburg
2100 Mshindi NF1 v Mshindi NF2
0 comments:
Post a Comment