by alanus
june2 2017
Ndugu
zangu, leo nimewakaribisheni ili kwa niaba ya Shikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) niweze kutoa shukrani zetu, pongezi na pia kutoa
mwelekeo wa timu zetu za vijana kuelekea Fainali za Kombe la Dunia mwaka
2026 (FIFA WORLD CUP 2026).
Timu
yetu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys
ilishiriki katika fainali hizi na kutolewa hatua ya makundi. Katika
hatua hii ilitoa sare ya 0-0 dhidi ya Mali, ikaifunga Angola bao 2-1 na
kutolewa kwa sheria ya uwiano wa matokeo (head to head) baada ya
kufungwa bao moja kwa bila na Niger.
Ni
jambo la kutia moyo kuwa bingwa wa mashindano haya Mali timu pekee
ambayo hawakuweza kuifunga ni Tanzania na timu nyingine zote
walizokutana nazo walizifunga ikiwemo na Ghana ambayo Serengeti Boys
walitokana nayo sare hapa Dar es salaam.
Hakika mashindano haya yameonyesha kuwa kumbe Tanzania tunao uwezo mkubwa wa kushindana katika mashindano makubwa.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania linapenda kutoa shukrani za pekee kwa
Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu,
Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa ambao kwa umoja wao walihakikisha timu
inawezeshwa kikamilifu na kuwa na nguvu kubwa ya kushindana.
Tunamshukuru
sana Mh Dk Harrison Mwakyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo pamoja na watumishi wa Wizara kwa ushirikiano na jitihada kubwa
walizozifanya kuhakikisha timu inapata maandalizi mazuri.
Tunawapa
hongera na kuwashukuru wachezaji wa Serengeti Boys kwa jitihada na
ukomavu wao katika kipindi cha maandalizi na cha fainali zenyewe.
Pongezi nyingi na shukrani kwa benchi la ufundi la timu na uongozi wa
timu unaoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF Ndugu Ayoub
Nyenzi, Kamati ya Utendaji ya TFF wakati wote ilikuwa karibu naye na
ilimpa nguvu sana. Hongera pia kwa wafanyakazi wa TFF waliohakikisha
wanaratibu shughuli za timu kwa ufanisi mkubwa.
TFF
inawashukuru sana wajumbe wote wa Kamati ya Uhamasishaji ya Serengeti
Boys iliyoongozwa na Bw Charles Hilary. Uhamishaji wao ulikuwa ni mkubwa
sana na uliamsha ari ya Watanzania kuhamasika na kushangilia timu.
Shukrani sana kwa wadau wote waliochangia timu na shukrani sana kwa
waandishi wa habari na wasimamizi wa blogu mbalimbali na ma admin wa
makundi mbalimbali ya mitandao waliohamasisha na kuichangia timu.
MPANGO WA BAADAYE WA SERENGETI BOYS.
Kikosi
hiki cha Serengeti Boys kilichoshiriki fainali hizi sasa kimebadilika
na kuwa rasmi timu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 20 NGORONGORO
HEROES. Timu hii mwaka kesho itashiriki katika hatua hatua za kufuzu
kucheza fainali za Afrika umri chini ya miaka 20 Afcon U20. Fainali hizi
zitafanyika mwaka 2019. Benchi la ufundi la timu hii linaandaa program
ya maandalizi ya kikosi hiki ambayo itahusisha kambi na mechi za
majaribio ndani na nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment