Mkutano wa mwaka kuhusina na mpira wa miguu umefanyika nchini China ukihudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo duniani kote.
Mkutano
huu una lenga kuwaweka karibu wawekezaji na taasisi mbalimbali za
mchezo huo wa mpira nchini humo, katika juhudi za kuendeleza fani hiyo
hiyo kimataifa, hususan kibiashara zaidi. China kwa sasa imekuwa ikiweka nguvu zake pia katika kuwekeza kwenye mpira wa miguu.Mkutano
huu wa mwaka umefanyika katika mji wa Guangzhou kuanzia Juni mosi na
mbili, ambapo wafanyabiashara katika masuala ya mpira wa miguu nchini
China wanajaribu kujifunza katika soko la kimataifa ili kuweza kuinua
kiwango cha soka nchini humo.Na pia kuwawezesha wawekezajji wa kigeni kuweza kufahamu kandanda la China.Mkutano
huo umefanyika katika mji huo wa Guangzhou kutokana na historia yake
katika masuala ya mpira ambako mwezi Juni mwaka 1954 timu ya kwanza ya
mpira wa miguu ya kiwango cha juu ilianzishwa na kupewa jina la
Zhongnan.
0 comments:
Post a Comment