details june3 2017
by alanus
Vijana wa Real Madrid wataingia katika mchezo huo wakihitaji bao moja tu ili kuweza kuwa timu ya kwanza kufunga idadi ya mabao 500 katika michuano ya Champions League.
Lakini haitakuwa rahisi kwa Real Madrid kufanya hivyo kwani Juventus hawajafungwa hadi sasa na wanataka kumaliza msimu huu wa champions league bila nyavu zao kuguswa.
Endapo Juventus wataifunga Real Madrid na kubeba ndoo itawafanya kuwa timu ya kwanza baada ya United ya mwaka 2008 kumaliza msimu wa champions league bila kufungwa.
Na Juventus wanakisasi na Real Madrid cha mwaka 1998 nchini Uholanzi ambapo Jeventus “The Biaconeri” walifungwa na Los Blancos katika fainali ya Uefa ya mwaka huo.
Hadi sasa hakuna mchezaji aliyefikia rekodi ya Paulo Maldini ya kufunga bao la mapema katika fainali ya champions league ambapo Maldini alitumia sekunde 51 kufunga katika mechi dhidi ya Liverpool mwaka 2005.
Lakini Massimiliano Allegri ameshashinda Coppa Italia na Serie A anahitaji Champions League ili kuwa sawa na Jose Mourinho,Pep Gurdiola,Jup Heyckens,Luis Enrique na Sir Alex Ferguson ambao wamewahi kubeba makombe matatu makubwa ndani ya msimu mmoja.
Endelea kusbscribe channel yetu ya YOU TUBE ya Dauda Tv kupata kwa ukaribu kabisa uchambuzi na takwimu muhimu kuelekea mchezo huu mkubwa kabisa.
0 comments:
Post a Comment