alanus
Kikosi cha wachezaji 22 wa timu ya
Tanzania ‘Taifa Stars’, kinaondoka leo Alhamisi Juni 22, 2017 kwenda
Afrika Kusini katika michuano ya kuwania Kombe la Castle Cosafa.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia
ya Serengeti, ilikuwa kambini Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa
Jamhuri katikati ya jiji la Dar es Salaam, tangu Jumapili Juni 18, mwaka
huu.
Taifa Stars imeandaliwa kwa
michuano hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za
Kusini mwa Afrika. Tanzania si mwanachama wa Cosafa, lakini imealikwa
katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu.
Taifa Stars imepangwa kundi A na
timu za Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji,
Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika
Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu
(play off) ili kuingia robo fainali.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Taifa
Stars, Salum Mayanga, kikosi kinachoondoka leo ni makipa Aishi Salum
Manula (Azam FC), Benno David Kakolanya (Young Africans SC) na Said
Mohammed Said (Mtibwa Sugar FC).
Walinzi wa pembeni upande wa kulia
ni Shomari Salum Kapombe (Azam FC) na Hassan Hamis Ramadhan ‘Kessy’
(Young Africans SC) wakati upande wa kushoto wapo Gadiel Michael (Azam
FC) na Amim Abdulkarim (Toto Africans FC).
Walinzi wa kati ni Erasto Nyoni
(Azam FC), Salim Hassan Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC)
na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) wakati viungo wa kuzuia kuwa ni Himid
Mao (Azam FC) na Salmin Hoza wa Mbao FC.
Kadhalika wako viungo wa
kushambulia ambao ni Mzamiru Yassin Selembe (Simba), Simon Happygod
Msuva (Young Africans SC), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza
Ramadhani Kichuya (Simba SC).
Katika safu ya ushambuliaji wamo
Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Abeid
Yusufu (Kagera Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na
Shabani Idd Chilunda (Azam FC).
0 comments:
Post a Comment