by alanus
TIMU
ya Manchester City inatarajiwa kuanza mazungumzo rasmi na beki Dani
Alves baada ya Juventus kuthibitisha itavunjiana naye mkataba.
Beki
huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 34 anatarajiwa kusaini mkataba wa
miaka miwili na City akaungane na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola
walipokuwa Barcelona akivunja mkataba na Juventus.
Akizungumza
na Calciomercato.com na Mediaset Premium, Mtendaji Mkuu wa Juventus,
Beppe Marotta alisema: "Si uvunjaji wa mkataba kwa utashi wetu, bali
matakwa ya mchezaji mwenyewe,".
Dani Alves atavunja mkataba wake na Juventus ili ahamie Man Cit akaungane tena na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola PICHA ZAIDI GONGA HAPA
"Dani
Alves ametuambia anataka kujaribu uzoefu mwingine, hivyo atavunja
mkataba kwa makubaliano ya kiungwana na tunamtakia kila la heri,".
"Ni kweli kuliwa kuna mambo ya kustaajabisha katika mazungumzo yake, lakini tunathibitisha hakukuwa na mgawanyiko,"alisema.
City imesema ilitaka kumuuza Nolito na wamesema Sevilla wapo karibu kumchukua kwa mkopo mshambuliaji huyo.

0 comments:
Post a Comment