KIKOSI
cha timu ya soka ya taifa ya wanawake Tanzania, Twiga Stars kitaingia
kambini Juni 7, mwaka huu kwa ajili ya kujiaandaa na michezo miwili ya
kirafiki dhidi ya timu za wanawake za Dubai na nyingine kutoka nchini
Kenya.
Akitangaza
kikosi cha timu hiyo leo, kocha Mkuu wa Twiga Stars, Sebastian Nkoma
amesema kwamba upande wa makipa ni Elina Julius, Najiat Abbas, Fatuma
Omary na Faraja Kimlola.Mabeki
ni Wema Richard, Christina Daudi, Maimuna Hamisi, Annastazia Anthony,
Silvia Mwacha, Esther Mayala, Eva Jackson, Sophia Mwasikili, Christina
Panklasi na Asfati Kasindo.
Viungo ni Dorisia Daniel, Grace Mbeyela, Amina Ally, Asha Hamza, Happy Hezron, Kevilis Kikumbi, Anna Hebron, Tatu Iddi, Stumai Abdallah, Herrieth Shija, Hamisa Athumani na washambuliaji Rehema Abdul, Asha Rashid ‘Mwalala’, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’, Veronica Mapunda, Fatuma Mustafa na Oppah Clement.
Kocha Seba amesema kikosi hicho kitakaa kambini kwenye hosteli za Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam kwa muda wa siku 12, kabla ya kuelekea mjini Arusha kwa ajili ya michezo hiyo ya kirafiki.

0 comments:
Post a Comment