by alanus
Baada ya Yanga kumsajisili Ibrahim
Ajibu kwa dau nono la shilingi milioni 50 pamoja na kumpa usajifiri wa
gari, sasa Simba nao wamejibu mapigo.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa mazungumzo baina ya kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima na Simba yamefikia pazuri.
Niyonzima ambaye amemaliza mkataba
wa kuitumikia Yanga hivi karibuni pia alikuwa katika mzungumzo ya
kusaini mkataba mpya kuendelea kuichezea Yanga lakini hawakuwa wamefikia
kwenye hatua nzuri.
Mtu wa karibu wa Simba ametoa
tamko hili baada ya kuulizwa juu ya tetesi hizo: “Ni kweli kaka
Niyonzima amesaini Simba miaka miwili kwa dau nono.”
Pamoja na hivyo, rafiki wa karibu
wa Niyonzima alipoulizwa juu ya suala hilo, amesema: “Siyo kweli bado
hajasaini Simba ila ni kweli alizungumza nao jana.”
0 comments:
Post a Comment