Timu ya Singida United
imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Rwanda ambaye alikuwa anacheza
timu ya Polisi,Danny Usengimana na kuwa mchezaji wa sita wa kigeni
kusajiliwa na matajiri hao.
Mshambuliaji huyu anayetabiliwa
kuwa nitishio katika kufumani nyavu ukanda wa Afrika Mashariki na Kati
ameingia kandarasi ya miaka miwili na kikosi cha Kocha Mkuu wa zamani wa
Mabingwa Ligi Kuu ya Tanzania bara Yanga ,Hans Van Der Pluijm.
Timu ya Singida United ni timu
tatu zilizopanda kushiriki Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara
na nyingine ni Lipuli pamoja na Njombe Mji.
0 comments:
Post a Comment