by alanus
KIUNGO
wa zamani wa Chelsea, Oscar jana alijikuta akigombewa kama mpira a kona
baada ya mechi kati ya timu yake, Shanghai SIPG na Guangzhou R&F
iliyoisha kwa sare ya 1-1.
Oscar
amekuwa akifurahia maisha tangu amejiunga na Shanghai Januari na
mwanasoka huyo wa kimataifa wa Brazil jana aliendeleza na kazi yake
China na kujikuta anapambana na wachezaji wawili Uwanja wa Yuexiushan.
Baada
ya kumsetia mchezaji mwenzake, Hulk kufunga bao la kusawazisha kipindi
cha kwanza, Oscar baadaye akapatwa na jazba na kuwababua na mpira kwa
mashuti mawili mfululizo wachezaji wa timu pinzani.

Wachezaji
wa Guangzhou nao wakakasirika na kumvaa kuanza kumshambulia Mbrazil
huyo kabla ya wahezaji wenzake Oscar wa Shanghai SIPG nao kwenda
kumsaidia mwenzao, hivyo kufanya vita ya mapigano ya watu wote 22
waliikuwa uwanjani.
Walitupiana
makonde kadhaa huku wachezaji wa Shanghai wakionekana kumsaidia Oscar,
ambaye alikuwa bado amelala chini ya kushambuliwa na wapinzani.
Baada
ya vurugu hizo kutulizwa na wachezaji hao kuachanishwa, Li Tixiang
alitolewa kwa kadi nyekundu sawa na Fu Huan, huku Oscar akinusurika
adhabu yoyote.
Baada
ya sare hiyo ya 1-1, Shanghai SIPG inabaki nafasi ya pili kwenye
msimamo wa Ligi Kuu ya China - ikizidiwa pointi nne na vinara Guangzhou
Evergrande.
0 comments:
Post a Comment