- Details by alanus
- Created: Wednesday, 12 July 2017 11:58
Baada ya kumkosa Kiungo wa Chelsea Nemanja Matic kwa sababu ya
'kuwapora' Romelu Lukaku, sasa Man United wapo njiani kuwasilisha Ofa ya
Dau la Pauni Milioni 40 kumnunua Dier.
Lakini Dau hilo lipo chini ya Pauni Milioni 60 ambazo Spurs ndizo wanazoona ndio thamani halisi ya Eric Dier mwenye Miaka 23.
Hata hivyo, Man United wanaamini watafikia muafaka na Spurs ingawa
wanamhofu Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy ambae ni mgumu mno kufanya nae
biashara.
Hilo lilionekana wakati Man United walipowanunua kutoka Spurs Michael Carrick Mwaka 2006 na Dimitar Berbatov Mwaka 2008 na dili hizo kukamilishwa kwa mbinde na kwa bei ghali mno.
Lakini safari hii presha ya Mchezaji mwenyewe Dier kutaka kuhama huenda ikawasaidia mno Man United.
Tayari Dier ameshawaambia Maswahiba wa karibu yake kuwa anafurahia kufanya kazi na Mourinho.
Pia, mvuto mkubwa kwake Dier kwenda Man United ni kuongezeka mno
kwa Mshahara wake kutoka Pauni 70,000 anazopata sasa huko Spurs na
kupanda hadi zaidi ya Pauni 150,000 atakazopata akijiunga na Man United.
0 comments:
Post a Comment