
Mchezaji wa Everton Yannick Bolasie
alipata mapokezi ya aina yake nchini Tanzani wakati timu hiyo
ilipowasili katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam nchini Tanzania kwa
mechi ya kirafiki.
Winga huyo wa Everton ambaye ni raia wa DR
Congo na ameifungia nchi yake mabao 8 na kuichezea mara 31, alipokewa
na mashabiki wake kwa shangwe wakiimba jina lake huku wakipeperusha
bendera za DR Congo.Baadaye mahabiki hao walilifuata basi la timu hiyo kwa kupanda pikipiki huku wakiendelea kuimba nyimbo za kumsifu.
- Klabu ya Everton kucheza nchini Tanzania
- SportPesa kusitisha udhamini Kenya
- Salim Kikeke: EPL imerejea, lakini nani watawika?
Kikosi hicho cha Ronald Koeman kinatarajiwa kuchuana na mabingwa wa
Sportpesa Gor Mahia katika mechi ya kirafiki siku ya Alhamisi.
0 comments:
Post a Comment