Baada ya mapumziko ya mwezi mmoja
ya Ligi Kuu Zanzibar, timu ya Okapi ya Msuka kisiwani Pemba imeanza
mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michezo yake ya ligi hiyo hatua ya
nane bora inayotarajiwa kundelea Julai 9 mwaka huu visiwani hapa.
Okapi inatarajiwa kushuka katika kiwanja cha Gombani kisiwani Pemba kumenyana na maafande wa JKU wakati wa saa 10.00 jioni.
Msemaji wa timu hiyo, Hamad
Sharia Juma alisema kuwa pamoja na kikosi chake kuanza mazoezi kidogo
kidogo katika kipindi cha Ramadhani, lakini hivi sasa mazoezi mazito
yanaendelea.
0 comments:
Post a Comment