BENO
Kakolanya, mlinda mlango namba mbili wa Simba ameonyesha ukomavu kwenye mechi
yake ya kwanza akiwa na Simba kwa kuvunja rekodi ya mlinda mlango namba moja Aish
Manula ndani ya dakika 90 za kwanza kukaa langoni bila kufungwa.
Kwenye
mchezo wa kwanza wa ligi kwa Manula kukaa langoni dhidi ya JKT Tanzania
alishindwa kutoka na Clean Sheet licha ya ushindi wa mabao 3-1 ila Kakolanya
ameanza kwa kutoruhusu bao huku timu hiyo ikishinda jumla ya mabao 4-0 dhidi ya
Lipuli na mechi zote zilichezwa uwanja wa Uhuru.
Kakolanya
amesugua benchi kwenye mechi 10 mbazo ni sawa na dakika 900 ambazo zote Manula
alikaa langoni na kufungwa jumla ya mabao matatu amepotezwa na Kakolanya kwenye
dakika 90 za mwanzo.
Kocha wa
makipa ndani ya Simba, Mwarami Mohamed amesema kuwa
makipa wote ni bora utofauti wao ni namba tu ndani ya kikosi.
“Makipa wote
wa Simba ni bora na watapata nafasi, tofauti ni kwamba Manula ni kipa namba
moja wa Simba kwa mengine wapo sawa na kila mmoja ana kitu chake cha pekee,”
amesema.
0 comments:
Post a Comment