MEDDIE
Kagere mshambuliaji wa Simba guu lake limeibuka uwanja wa Uhuru baada ya kupita
dakika 229 alizocheza bila kuzifumania nyavu kwenye mechi mbili alizocheza
akiwa na Simba msimu huu.
Kagere
amefunga mabao tisa mpaka sasa ni mabao matano amefunga kwa guu la kulia huku
mawili akifunga kwa guu la kushoto na mawili kwa kichwa mara ya mwisho kufunga
ilikuwa mbele ya Mbeya City wakati Simba ikishinda mabao 4-0 akifunga kwa guu
la kulia kwa penalti iliyosababishwa na Miraj Athuman ‘Sheva’.
Alicheza
dakika 229 bila kufunga bao mbele ya Tanzania Prisons mchezo ulokamilika kwa
sare ya bila kufungana pia kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting
hakufunga mpaka alipoifunga Lipuli dakika ya 49 na kufanya zitimie dakika 229
bila kufunga kwenye ushindi wa mabao 4-0 uwanja wa Uhuru.
Timu
nyingine ambazo Kagere amezifunga ni pamoja na JKT Tanzania wakati Simba ikishinda mchezo
wake wa kwanza mabao 3-1 alipachika mawili kwa guu lake la kulia akimalizia
pasi za mwisho za Mzamiru Yassin, mbele ya Mtibwa Sugar alipachika bao moja
kwenye ushindi wa 2-1 kwa pasi ya Sharaf Shiboub.
Mawili
alifunga mbele ya Kagera Sugar ambapo bao moja alifunga kwa kichwa akimalizia
pasi ya Shomari Kapombe na moja kwa penalti iliyosababishwa na Miraj kwa guu
lake la kulia.Lingine la kichwa alifunga mbele ya Azam FC uwanja wa Taifa
kwenye ushindi wa bao moja akimalizia pasi ya Francis Kahata.
Pia
aliifunga Biashara United kwa guu lake la kushoto akimalizia pasi ya Miraj
wakati Simba ikishinda mabao 2-0 uwanja wa Karume na bao lake la nane ilikuwa
kwenye ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Mbeya City na bao lake la tisa alifunga
kwa guu la kulia kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Lipuli.
Kagere
ameliambia Championi Jumamosi kuwa kila siku anajipa changamoto mwenyewe ili
kuwa bora.
0 comments:
Post a Comment