Saturday, July 8, 2017

by alanus
 Pedro Obiang

Kiungo wa kati wa West Ham United Pedro Obiang ametia saini mkataba mwingine wa miaka mitano katika klabu hiyo.
Obiang, 25, alikuwa mchezaji wa kwanza kununuliwa na meneja Slaven Bilic alipojiunga na klabu hiyo, ambapo alinunuliwa kutoka Sampdoria mwaka 2015.
"Kwa miaka mitano ijayo, tunaweza kutimiza mambo mengi, mambo mengi," mchezaji huyo wa zamani wa timu ya wachezaji wa chini ya miaka 21 wa Uhispania amesema.
Yeye ndiye mchezaji wa pili wa klabu hiyo kutia saini mkataba wa muda mrefu katika klabu hiyo katika kipindi cha wiki moja, baada ya Angelo Ogbonna pia kutia saini mkataba wa miaka mitano.

0 comments:

Post a Comment