Tuesday, July 4, 2017


Mdau mkubwa wa soka la Bongo amesema, anafatilia michuano ya Ndondo Cup na yeye ni shabiki wa kutupwa wa Kauzu FC huku akivutiwa zaidi na Chief wa Kauzu kutokana na aina yake ya ushangiliaji.
“Nimeshuhudia mechi nyingi za Ndondo, nimeona hata washangiliaji wanaokuja ni viwanjani ni wastaarabu sana. Mimi ni shabiki wa Kauzu FC navutiwa sana na yule mzee anaebebwa ‘Chief wa Kauzu’,” Rage wakati anazungumzia michuano ya Ndondo Cup.
“Clouds Media wanastahili sifa, wanapoandaa mashindano kama haya na yanachukua muda mrefy, wanapunguza muda wa vijana kufanya mambo yasiyofaa kama kujihusisha na uvutaji wa bangi vijiweni na kuona sio kitu muhimu.”
Rage amesema, enzi zake amekipiga sana mechi za Ndondo na amesimulia uzoefu wake katika mechi za Ndondo katika kipindi chao.
“Ndondo inanikumbusha mbali sana Ndondo Cup, sisi pia tulikua na mashindano yetu, utakuta sisi Simba mchezaji wetu na nahodha Haidary Abeid Muchacho na Khalid Abeid walikua walikua na timu yao inaitwa Poliengland ilikua maeneo ya Gerezani. Sisi ambao tulikua tunakaa Kariakoo tulikua na timu yetu inaitwa Saigon.”
“Akina marehemu Chogo, Abdallah Kibaden, walikua na timu yao Young Kinya, kuna wengine walikuwa Good hope Temeke. Kwa hiyo tulikuwa tunatoka kwenye klabu zetu tunaenda kucheza kwenye timu zetu za mitaani.”
“Na wakati huo tulikuwa na marefa wetu akionesha penati basi anaonesha kwa kisu, anatoa kisu hapa penati inapigwa pale ili usimsogelee. Kulikuwa na ubabe sana wakati ule.”
Rage ni miongoni mwa wadau wa soka nchini ambaye alishuhudia baadhi ya mechi  za msimu uliopita kwenye uwanja wa Chuo cha Utalii zamani Bandari uliopo maeneo ya Tandika.

0 comments:

Post a Comment