by alanus
Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF jana ilivunja Kamati ya
uchaguzi na kuteua Kamati nyingine kusimamia uchaguzi huo.
Uamuzi
huo ulitokana na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Msomi
Revocatus Kuuli kutumia mamlaka yake kisheria na kuamua kusimamisha
mchakato wa uchaguzi baada ya kutokea kutokuelewana ndani ya Kamati
hiyo.
Kwa
mujibu wa maelezo ya Wakili Msomi Kuuli aliyoyatoa baada ya kutokea
kutokuelewana huko wajumbe walitofautiana kwa kutaka kuwakata wagombea
bila sababu za msingi na kutaka Rais wa TFF Jamal Malinzi apitishwe bila
kufanyiwa usaili.
Kutokana
na utata huo, Kamati ya Utendaji ya TFF iliamua kuwafuta wajumbe wa
Kamati mbalimbali ikiwemo Kamati ya uchaguzi na kumuacha mwenyekiti wake
Wakili Msomi Kuuli.
Wajumbe
walioenguliwa kwenye Kamati ya uchaguzi ni Wakili Msomi Domina Madeli
aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Juma Lalika, Jeremiah Wambura na Omary
Hamidu.
Wajumbe
wapya walioteuliwa kuungana na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Wakili
Msomi Kuuli ni Wakili Msomi Mh Mohammed Mchengela (MB), Wakili Msomi
Malangwe Ally, Wakili Msomi Kilomoni Kabamba na Wakili Msomi Deus Kalua.
Nimesikitishwa
na kitendo cha mgombea mwenzangu urais wa TFF, Wallace Karia kushiriki
mchakato wa uchaguzi kwa kuongoza kikao cha Kamati ya Utendaji
kilichoteua wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi.
Karia
ana mgongano wa maslahi katika suala zima la uchaguzi kwa sababu naye
ni mgombea wa nafasi nyeti ya urais. Katikati ya mchakato wa uchaguzi
anaposhiriki kuongoza kikao kinachoteua Kamati ya Uchaguzi ni suala
ambalo linaashiria kutokuwepo kwa haki katika mchakato mzima.
Msimamo
wa kisheria unahitaji sio tu kwamba haki itendeke, bali pia ionekane
imetendeka. Kama mtakumbuka Bw. Karia aliwekewa pingamizi la uraia wake.
Anaposhiriki
kama kiongozi mkuu kufuta Kamati iliyokuwa inajadili pingamizi juu ya
uraia wake na kuunda nyingine inatoa picha ya kuwapo nguvu ya ziada
katika kusukuma mchakato wa uchaguzi.
Katika
mazingira kama haya hata kama haki itatendeka, haiwezi kuonekana kama
imetendeka. Hii ni dosari kubwa sana kwenye huu uchaguzi.
Nafahamu
kwamba Kamati ya Utendaji imetumia mamlaka yake kikatiba kufuta na
kuunda Kamati mpya ya Uchaguzi pamoja na Kamati nyingine.
Lakini
wajumbe wengi wa Kamati ya utendaji ni wagombea. Wameenda kuteua Kamati
itakayoshiriki kuwachuja. Huu ni ubabaishaji mwingine ndani ya mpira wa
miguu Tanzania.
Busara
ya kawaida ilikuwa inahitaji Kaimu Rais Karia akiri mgongano wa maslahi
(declaration of conflict of interest) na kujitoa katika mchakato huo.
Nawaomba
ndugu zangu kama tunataka kuleta mabadiliko ya kweli katika kuendesha
mpira wa miguu inabidi tusikubali ubabaishaji wa aina hii katika mpira.
Bila
hivyo tunaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu kila kukicha kwa sababu
watendaji wetu wanafanya hila kutekeleza matakwa yao kuanzia kwenye
UchaguZi.
Mtu
ambaye anasimamia figisu katika mchakato wa uchaguzi ama kwa rushwa au
kwa njia nyingine yoyote tusitarajie uongozi bora kutoka kwake.
Kamati
ya Uchaguzi ingetengenezwa kwa mazingira huru, ingeachwa ifanye kazi
yake kwa uhuru na wajumbe wangeachwa wafanye maamuzi yao kwa uhuru bila
vishawishi vya rushwa wala upendeleo hapo tungeweza kupata viongoZi bora
katika kuendesha mpira wa miguu.
Vyanzo
vya matatizo ya uongozi katika mpira huwa vinaanzia kwenye uchaguzi.
Tuache ubabaishaji. Tutengeneze mchakato wa haki ili kupata viongoZi
bora watakaoweza kusimamia mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa mpira
watu.
*SHIJA RICHARD SHIJA*
*MGOMBEA WA NAFASI YA URAIS UCHAGUZI MKUU TFF*
*JULAI 05, 2017.*
0 comments:
Post a Comment