by alanus
Ibrahim Ajib ametambulishwa
rasmi na klabu ya Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili
kuitumikia klabu hiyo kwenye mashindano mbalimbali kuanzia msimu wa
2017-2018.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles
Bonifasi Mkwasa na meneja wa timu Saleh Hafidh wamemtambulisha Ajib
mbele ya waandishi wa habari ndani ya makao makuu ya Yanga mtaa wa
Jangwani.
Awali zilianza kama tetesi huku
Ajib na Yanga wote wakikanusha tetesi ambazo zilikua zikiibuliwa kwamba
Ajib amesaini mkataba na Yanga.
Ajib amekabidhiwa jezi namba 10
ambayo ilikuwa inavaliwa na Matheo Anthony, Ajib ameondoka Simba akiwa
anavaa jezi namba 23 ambapo kwa upande wa Yanga jezi hiyo inavaliwa na
nahodha Nadir Harou ‘Cannavaro’.
0 comments:
Post a Comment