WACHEZAJI
wa Barcelona na benchi lao la Ufundi, leo walilazimika kusimama kimya
kwa dakika moja kabla ya mazoezi yao ili kuwafariji watu waliokufa
katika milipuko ya kigaidi mjini humo.
Mashambulio
mawili ya gari mjini Barcelona nja ukanda ewa bahari mjini Cambrils
Alhamisi na mapema Ijumaa asubuhi yamechukua uhai wa watu 14, huku
wengine wapatao 130 wakijeruhiwa.
Polisi
wamewapiga risasi na kuwaua watu watano waliojivalisha mabomu feki
baada ya shambulio la Cambrils, wakati dereva wa basi dogo lililotumika
kwenye shambulio la Barcelona bado hajapatikana.
Mapema
tu Barca ilithibitisha wachezaji wake watafunga vitambaa vyeusi
mikononi kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa msimu mpya wa La Liga dhidi ya
Real Betis Uwanja wa Nou Camp Jumapili.
Real
Madrid nao walitulia kwa dakika moja kabla ya kuanza mazoezi ya Ijumaa,
kufuatia mashambulio mawili ya kigaidi nchini Hispania.
Real
wanatarajiwa kuanza kampeni ya kutetea taji lao Ligi Kuu ya Hispania,
maarufu kama La Liga ugenini dhidi ya Deportivo La Coruna Jumapili
Wakati huo huo: Kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola ambaye kwa sasa anafundisha
Manchester City naye ametoa pole kwa tukio hilo.

0 comments:
Post a Comment