KLABU
ya Barcelona imetangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji chipukizi,
Ousmane Dembele kutoka Borussia Dortmund kwa dau la Pauni Milioni 96
ambalo linaweza kuongezeka.
Klabu
hiyo ya Katalunya imethibitisha habari hizo katika ukurasa wake wa
Twitter ikiweka na picha ya Dembele akiwa na jezi ya Barca na katika
taarifa nyingine kwenye tovuti yao wamemuita 'mmoja wa wachezaji bora
barani'.
Anawasili
kuziba pengo lililoachwa na Neymar, aliyehamia PSG mapema mwezi huu kwa
dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 198 na Dembele atakuwa anavaa
jezi namba 11 iliyoachwa wazi na Mbrazil huyo aliyeondoka.
Barcelona imetangaza kumsajili Ousmane Dembele kutoka Borussia Dortmund PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Dau
la Pauni Milioni 96 linamaanisha Dembele atakuwa mchezaji wa pili ghali
kihistoria baada ya Neymar na klabu itakayotaka kumnunua mchezaji huyo
italazimika kuipa Barca Pauni 368.
Barcelona
imesema Dembele atawasili Hispania Jumapili kwa ajili ya kufanyiwa
vipimo Jumatatu kabla ya kutambulishwa mapema wiki ijayo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 aliibukia Rennes ya Ufaransa, kabla ya kujiunga na timu ya Bundesliga msimu uliopita.
Dembele
amefunga mabao 10 katika mechi 49, na anashika nafasi ya tatu Ulaya kwa
kutengeneza nafasi za kufunga, akiwa ameseti mabao 20 katika mashindano
yote.
Haijulikani
kama baada ya Barcelona kumpata Dembele itaendelea na mpango wa
kumsajili kiungo Mbrazil wa Liverpool, Philippe Coutinho baada ya ofa
zake nne kukataliwa Anfield au la.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa sasa anasumbuliwa na maumivu ya mgongo
na kuumwa kwake kumekuza tetesi za kuondoka ingawa ameitwa hivyo hivuo
katika timu yake ya taifa, Brazil kwa ajili ya mechi zijazo.
Kocha
wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema leo kuhusu Coutinho kwamba: "Kwa
sasa yupo kwenye orodha yetu ya majeruhi, hivyo ndivyo ilivyo na
haijabadilika. Sijui. Sijawasiliana na FA ya Brazil kwa sasa, lakini
sheria ni kama wanataka kumuona na kumuangalia anapaswa kwenda huko,".

0 comments:
Post a Comment