Asubuhi ya leo ndio lile pambana la ndondi lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa kati ya bondia Floyd Money Mayweather na bingwa wa UFC Conor McGregor ilimepigwa.
McGregor alifanikiwa kwenda hadi katika raundi ya 9 lakini ilipofika raundi ya 10 mambo yalibadilika baada ya Mayweather kumshambulia sana hadi Gregor aliyekuwa hoi sana huku ikiwa imebaki dakika 1:55 kwa pambano kuisha.
Baada ya raundi ya 4 kuisha na Gregor kuonekana mchangamfu, kibao kilianza kubadilika raundi ya 5 ambapo alianza kuonekana kuchoka na ilipofila ya 8 McGregor alionekana hoi zaidi ndipo ya 10 alishambuliwa sana akiwa hoi bina taaban.
Baada ya mchezo huo Floyd alisema “nimewapa mashabiki kile walichotaka kukiona, baada ya mpambano ya Pacquao niliwaahidi kwamba nitarudi kuwafurahisha na leo wameona nilichofanya” alisema Mayweather huku akisisitiza “ni mpambano wangu wa mwisho.
0 comments:
Post a Comment