Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa
Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga amemwongeza Kiugo wa
Young Africans, Emmanuel Martin kwenye kikosi chake kinachojindaa
kucheza na Botswana Jumamosi Septemba 2, mwaka huu.
Mchezo huo wa kirafiki wa
kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam chini ya
utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA).
Emmanuel Martin anatarajiwa
kujiunga na kambi ya Taifa Stars mara moja leo Agosti 30, mwaka huu na
kuanza na mazoezi na wenzake yatakayofanyika jioni kwenye Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam.
Emmanuel Martin ameongezwa na
Mayanga baada ya mawasiliano kuonesha kwamba huenda akawakosa nyota wa
kimataifa Simon Msuva kutoka Difaa El Jadidah ya Morocco na Orgenes
Mollel wa FC Famalicao ya Ureno.
Taarifa kutoka Morocco inaonesha
kwamba Msuva ana kibali cha muda cha kuingia na kutoka Morocco ‘visa’
ambacho kinamnyima haki ya kutoka na kuingia Morocco mara kwa mara.
Kuna juhudi zinafanywa na timu
yake kadhalika Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco kumfanikishia
kupata kibali cha muda mrefu ili iwe rahisi kwa mchezaji kutoka na
kuingia kama anahitaji katika timu ya taifa.
Kuhusu Mollel taratibu za ruhusa
za kimataifa zinafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria za nchi ya Ureno
ambako anacheza soka la kulipwa.
Nyota wengine wote wameripoti
Taifa Stars wakiwamo wale wa kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kama vile
Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Elias Maguli (Dhofar FC/Oman), Abdi
Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya)
wakati Farid Mussa wa CD Tenerif ya Hispania anatarajiwa kutua leo.
Wengine ambao wako kambini Hoteli
ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam ni makipa Aishi Manula
(Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young
Africans).
Pia wamo Walinzi ni Gadiel Michael
(Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young
Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo ni Himid Mao – Nahodha
Msaidizi (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC),
Shiza Kichuya (Simba SC), wakati Washambuliaji ni Raphael Daud (Young
Africans) na Kelvin Sabato (Azam FC).
Benchi la Ufundi la Mayanga
linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha
Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja),
Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa
Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
0 comments:
Post a Comment