Sunday, September 3, 2017

Mara baada ya ushindi wa magoli 2-0 ilioupata Taifa Stars dhidi ya Botswana September 2, 2017 nahodha wa Stars Mbwana Samatta amesema, hakukuwa na namna yoyote kwa Botswana kukwepa kufungwa kwa sababu kikosi cha Stars kilikuwa bora kuliko wao.
“Botswana walijitahidi kujaribu kuzuia kufungwa lakini ilikuwa lazima wafungwe nadhani hawana kikosi bora kuliko Tanzania, tulikuwa bora na tumewafunga na hilo ndio ilikuwa inabidi litokee kwa hiyo walijitahidi lakini hawakuwa na nguvu ya kutufunga. Mimi nafikiri ilikuwa lazima wafungwe kwa sababu tuko vizuri,” Samatta.
Watu waliohoji kwamba Samatta hakuonekana katika ubora wake aliozoeleka amewajibu kwa kusema, mwalimu anaanda timu hamuandai mchezaji mmoja, kitu muhimu ni timu kushinda mechi bila kuangalia nani amecheza kwa kiwango gani.

0 comments:

Post a Comment